Habari jamani, wacha niende moja kwa moja, mimi na mwanamke na nimeolewa, na nina rafiki yangu tunashibana sana lakini nilikuja kugundua kitu ila nashindwa nafanyaje kuhusu hilo jambo, yaani iko hivi.
Yani hivi karibuni, na sio tu karibuni, ni tangu mwaka jana niligundua kua huyu rafiki yangu anatembea na mume wangu tena wanakutana mara kwa mara na maeneo tofauti tofauti na wote hawajioneshi kwangu kama wanamahusiano.
Lakini shida inakuja hapa sasa, ni kweli nimegundua hilo, lakini kiukweli na mimi mwenyewe natembea na baba wa huyu rafiki yangu, na baba yake ni amefanikiwa sana yaani anapesa nyingi za kutosha, na hua ananisaidia sana karibia kila mwezi ananiwekea pesa za kujikimu nyingi tu.
Sasa nikisema niwaambie kua najua wanamahusiano yaani mume wangu na huyu rafiki yangu, nahofia itakuja niharibia mambo yangu na baba yake huyu rafiki yangu, yani sijui nifanyeje, mume anauma ndio lakini sitaki kumuacha huyu baba yetu, anajua kutunza na ananipatia pesa kila mwezi.
Na najua kua rafiki yangu hajui kama mimi natembea na baba yake, na nahofia nikiharibu urafiki wetu nahofia huyu mbaba wangu atanikataa na mimi sababau anampenda sana binti yake na anamjali sana binti yake. Kwahiyo nikimpoteza tu huyu rafiki yangu basi na pesa ndo zinapotea, sijali kua kweli nampa utamu baba wa rafiki yangu, kikubwa matunzo ni mazuri sana.
Kuhusu mume wangu, nampenda sana, tena tuna watoto watatu pamoja. Hua najisikia kama kusalitiwa sababu huyu ni mume wangu anatoka na rafiki yangu, lakini na mimi nafanya hicho hicho kwa baba wa rafiki yangu.
Nilijuaje kuhusu mahusiano yao sasa, kuna siku wote wawili walikua hawaokei simu zangu, nikawa najiuliza kulikoni, kwahiyo nikachunguza mahali alipo yaani location sababu wote tunaoneshana mahali tulipo kwa usalama kama marafiki, na nilivyofatilia, nikawakuta wamekaa kwenye mgahawa kwa nje wanapata chakula cha mchana pamoja.
Nikashangaa kumuona rafiki yangu na mume wangu, nikajiuliza hivi mbona hana heshima, anawezaje kukaa na mume wangu kwa siri na asijibu simu yangu, sikuwastua wala, niliwaangalia tu kwa mbali, na baadae walitoka na kwenda kwenye hoteli moja na kuingia ndani, nilijaribu kuwapigia tena hawakujibu simu zangu basi nikaachana nao na kurudi zangu nyumbani.
Wakati huo lakini mimi nilishaanza mahusiano na baba yake rafiki yangu, ilikua tu siku tumekaa kwao, rafiki yangu aliniacha nyumbani kwao yeye alitoka kwenda kuchukua kitu, hapo ndipo baba yake akanifata na kuanza kuniongelesha mambo ya mapenzi, nilishangaa mwanzoni na kujizuia kutomwambia maneno mabaya, lakini alichukua namba yangu na aliendelea kunitongoza karibia kila siku.
Sikutaka kumwambia rafiki yangu kwakua ingeleta picha mbaya, baada ya muda nikaamua tu nimalizane nimpe anachokitaka yaani penzi ili asiendelee kunisumbua, hee bana bana, baada ya kufanya nae mapenzi si ndo huduma zikaanza moto moto, yaani anatuma pesa ya maana tu kila mwezi, hata kumuacha imekua ngumu. ndo maana hata nilivyowaona mume wangu na rafiki yangu wanaenda hotelini wala sikutaka kuyavuruga kwanza yaani sijui cha kufanya.
Na ni mara nyingi tu nikiona simu zangu hawapokei, najua tu wapo pamoja, nafikiri naacha iendelee hivyo hivyo, wivu upo ndio lakini wacha iwe siri maisha yanendelee, mimi natoka na baba mtu, na rafiki yangu anatoka na mume wangu.. maana sina lakufanya hapo kwakweli...
Keep reading
Sign in to read the full confession
Create an account or log in to unlock the rest of this story.