Habari familia... tafadhali, nahitaji ushauri. Mimi ni mwanaume niliyeoa, nina umri wa miaka 43. Kwa miezi michache sasa, nilianza mahusiano ya siri na wasichana wadogo wa pembeni, kwa ajili ya kupumzika.
💔Yule niliyenaye sasa ni binti mdogo anayefanya mafunzo kazini (intern) na penzi letu ni la moto sana. Kwa kweli, niliweza kusimamia vizuri sana jambo hili «ndani yaani mke wangu» na «nje yaani huyu mrembo wa pembeni», kila mtu alikuwa anafurahia.
Kila mwaka, huwa tunapiga picha kubwa ya familia nyumbani ambayo tunaweka sebuleni, na mwaka unaofuata ndipo tunaiondoa na kupiga mpya—ni utamaduni nyumbani kwetu na kwa familia yangu yaani mke wangu na watoto.
Sasa mwaka 2025, tulipiga picha tarehe 18 Desemba. Tarehe 20, mke wangu alipokea picha hizo na kuziweka nyumbani kama kawaida. Nilipoingia sebuleni jioni (baada ya kazi) nikiwa nimechoka sana, niliiona picha kubwa ya familia sebuleni na nikagundua kua kuna sura mpya imeongezwa (imebandikwa) kwenye picha ya familia.
Ilikuwa ni moja ya picha iliyomuonesha juu mpaka chini yaani kamili mpenzi wangu wa pembeni na ni ya wasifu wa Facebook, na mke wangu aliibandika kwenye picha pembeni yangu. Moyo wangu ulistuka sana hata hata ubongo wangu haujaelewa kinachoendelea.
Na kumbuka tayari nina matatizo ya moyo, siwezi kuhimili hisia kali za ghafla, na wakati huo nilipata shambulio dogo la moyo. Kuanzia tarehe 20 hadi 23, nilikuwa hospitalini. Mama yangu alipofahamu hili, mvutano uliongezeka zaidi.
Alimkemea mke wangu aache mambo ya kitoto, kwamba hatutatui matatizo kwa njia hii, n.k... Kwamba mke wangu anajua nina matatizo ya moyo lakini bado akaamua kufanya kitu kama hiki, n.k. Kwa kifupi tu ni kwamba, kuna mvutano kati ya mke wangu na familia yangu, na sitaki hilo liendelee.
Nataka kutuliza mambo, lakini mke wangu amekua mgumu sana na hataki kabisa kuonesha ushirikiano. Nilimuomba mke wangu anisamehe sana, nikasema natambua makosa yangu na nikamsihi aondoe hiyo picha sebuleni. Akaniambia hiyo picha itaondoka sebuleni Desemba 2026. Na tena, anaendelea na uchunguzi na amesema atazichapisha mitandaoni picha hizo kama akigundua kuwa naendelea kumsaliti, na atachukua picha ya mpinzani wake na kuiweka kwenye picha ya familia ya kuisambaza mitandaoni.
Analisimamia sana hili jambo: hatoi hiyo picha na nikitaka kuitoa ni ugomvi mkali!. Siwezi kuvumilia kuona hiyo picha: watoto wangu wananiuliza kuhusu hiyo sura mpya iliyoongezwa, hata watu wageni wanauliza, yaani ni aibu. Ina maana picha itabaki hapo na kila siku nikirudi kazini nitaiona? Je, hii ni kuniua au nini?! Natambua makosa yangu kweli nilimsaliti, lakini pamoja na haya yote, sitaweza kumtuliza mke wangu ilihali nimemsihi sana anisamehe na tena anaendelea kusisitiza kua hatatoa hiyo picha hata baada ya kumuomba kwa heshima aondoe picha hiyo.
Sitaki kufikia kufanya hatua za mbali sana vya ajabu. Nataka ushauri wa jinsi ya kulimaliza hili swala kwa utulivu. 😭💔😭🙏
Keep reading
Sign in to read the full confession
Create an account or log in to unlock the rest of this story.