Jamani yaliyonikuta hapana kweli, ni majonzi majonzi na sijui nifanyaje, mimi ni mwanamke na nina miaka 43 sasa na nina watoto watatu niliowahi kuzaa. sasa ipo hivi, kipindi nipo shule mdogo mdogo nilipata ujauzito, ikanisumbua sana na hali ya nyumbani haikua nzuri kifedha, basi yalikua mateso sana. na hata nilivyojifungua, nikiwa na miaka 16 hivi, nilishindwa kumuhudumia huyu mtoto kwakua nilikua mdogo na sikua na msaada wowote ule.
siku moja alikuja mwanamke mmoja akasema amempenda mwanangu na angetaka amlee yaani anisaidie, akanikaribisha hadi kwake, wanakaa sehemu nzuri sana.
nikasema mungu amenisaidia, wakati huo sijaendelea na masomo yangu, basi nikakaa nae pale kama miezi sita, siku moja niliamka asubuhi sikuona mtu mule ndani, mwanangu wala huyo mwanamke, yaani hakukua na mtu. niliita kila kona lakini wapi, niliulizia kwa majirani kila kona hakukua na mtu ameona chochote.
moyo wangu ulihuzunika sana na niliumia sana kwakile kitendo, nililia sana nikaona kama dunia nzima inaniangukia, mpaka ilifika kipindi nilitamani kuondoa maisha yangu, sababu kwenye ile nyumba sikukaa hata siku tatu wakaja watu wamesema wamepangishwa na mtu anakaa nje ya nchii hivyo walinitaka niondoke mule ndani mara moja.
ningefanya nini na sina mtetezi, nililia sana kama mwezi mzima nikiwa mtaani na kubangaiza na kupata nauli ya kurudi nyumbani. Wazee waliuliza kilichotokea, nikawaambia, walihuzunika sana, lakini hakukua na chakufanya sababu hali ilikua duni.
basi miaka ikaenda, mihangaiko ikaendelea na yale mawazo ya kumtafuta mwanangu yalipotea, nikapata kazi nzuri na kipato kikawa kizuri, hapo ni baada ya miaka 18, basi nikampenda kijana mmoja, sema alikua mdogo lakini mwili wake ulinivutia na nikaanza nae mahusiano.
alikua akikaa kwangu, uzuri alikua akijituma na kupambania masomo yake ya chuo na akikwama kifedha namsaidia, kiukweli alinipa faraja sana. na haikuchukua muda nipata mtoto wa kwanza nae wa kiume.
maisha yaliendelea, na baada ya kama miaka miwili mbele tukapata mtoto wa pili, wakiume pia. na alikua amepata kazi na yeye anaingiza kipato. ingawa nilikua nimemzidi umri sana tu lakini nilijisemea mapenzi sio umri. tukaendelea kulewa watoto wetu, maisha yaliendelea.
Sasa siku moja tukiwa chumbani tunajiliwaza, huyu baba watoto wangu akaanza kusimulia mambo ambayo mama yake alikua akimsimulia akiwa mdogo, alimwambia kua yeye sio mama yake na kua alitaka kumtafuta mama yake halisi lakini alishindwa ila akamwambia jina la mama yake ambalo lilikua jina langu la huko kwetu, maana tangu nianze ajira na masomo ya chuo jina nilitumia tofauti kabisa.
nilivyosikia vile, moyo ukapasuka paaa, yaniii nilibaki mdomo wazi, nikamuuliza baadhi ya maswali na kumtajia jina la huyu mama yake aliyemlea la ndani alilokua anatumia nyumbani, ndo akasema ni mama yake huyo.. aisee nilihisi kuchanganyikiwa, nikamwambia tukapime vipimo vya DNA.
tulienda na kuvipima, na baada ya kama wiki tatu tukapata majibu, bwana bwana kumbe alikua mwanangu yulee ambaye alitoroshwa na yule mama aliyesema atanisaidia, roho iliniuma sana, yaani kuzunguka kote nakuja kuzalishwa tena na mwanangu mwenyewe, nilichoka sana, na kijana hana cha kufanya, hajui aite mama au mkewe, yani sijui tunafanyaje, na watoto ndo hawa, wawili na umri ndo huo umesonga.
basi hayo ndo yanayonisibu, uzuri tupo pamoja na tunaendelea kuishi tu kama baba na mama kwa maana hatuna vya kuvificha, kama mapenzi tumeshafanya sana na tumezaa watoto, ila tumeiweka kama siri isije sikika kwa mtu yoyote lakini mimi nimeona niyatoe sehemu nione kama nitapata mawazo mengine. samahanini kwa gazeti refu maanaa..
Keep reading
Sign in to read the full confession
Create an account or log in to unlock the rest of this story.